Isaiah 3:4-12


4 aNitawafanya wavulana wawe maafisa wao,
watoto ndio watakaowatawala.
5 bWatu wataoneana wao kwa wao:
mtu dhidi ya mtu, na jirani dhidi ya jirani yake.
Kijana atainuka dhidi ya mzee,
mtu mnyonge dhidi ya mtu mwenye heshima.

6Mtu atamkamata mmoja wa ndugu zake
katika nyumba ya baba yake na kusema,
“Unalo joho, sasa uwe kiongozi wetu,
tawala lundo hili la magofu!”
7 cLakini siku hiyo atapiga kelele akisema,
“Sina uponyaji.
Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu,
msinifanye niwe kiongozi wa watu.”

8 dYerusalemu inapepesuka,
Yuda inaanguka;
maneno yao na matendo yao ni kinyume na Bwana,
wakiudharau uwepo wake uliotukuka.
9 eNyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao,
hujivunia dhambi yao kama Sodoma,
wala hawaifichi.
Ole wao!
Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.

10 fWaambie wanyofu itakuwa heri kwao,
kwa kuwa watafurahia tunda la matendo yao.
11 gOle kwa watu waovu! Maafa yapo juu yao!
Watalipwa kwa ajili ya yale mikono yao iliyotenda.

12 hVijana wanawatesa watu wangu,
wanawake wanawatawala.
Enyi watu wangu, viongozi wenu wanawapotosha,
wanawapoteza njia.
Copyright information for SwhNEN